Siku kama ya leo miaka 51 iliyopita
inayosadifiana na tarehe 15 Khordad 1342 Hijria Shamsia sawa na tarehe 5
Juni 1963 Milaadia, wananchi Waislamu wa Iran walifanya maandamano
makubwa dhidi ya utawala wa Shah, baada ya kusikia habari ya kutiwa
mbaroni Imam Khomeini MA. Imam alitiwa mbaroni na vibaraka wa utawala wa
Shah siku kadhaa nyuma kufuatia hotuba yake ya kihistoria aliyoitoa
katika mji wa Qum, ambayo ilifichua njama mbalimbali za utawala wa Shah
dhidi ya taifa la Iran. Ni wazi kuwa mapambano ya umwagaji damu na ya
kihistoria ya tarehe 15 Khordad, yalikuwa nukta ya kuanza mapinduzi ya
wananchi wa Iran dhidi ya utawala wa Shah na kufungua njia ya mustakbali
wa kisiasa na kijamii nchini.
--------------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita,
sawa na tarehe 5 Juni 1972, lilifanyika kongamano la kwanza la mazingira
huko Stockholm nchini Sweden. Kongamano hilo liliwashirikisha
wawakilishi 1300 kutoka nchi 113 duniani likiwa na kauli mbiu isemayo
'Kuna Ardhi Moja tu'. Miongoni mwa malengo makuu ya kongamano hilo
yalikuwa ni kuwekwa mikakati ya kujenga makaazi ya raia kwa kuzingatia
ulindaji mazingira, kuainisha na kudhibiti mada haribifu kwa mazingira
na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vya baadaye.
----------------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 47 iliyopita
muwafaka na tarehe 5 Juni 1967, vilianza vita vikubwa vya tatu kati ya
utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu. Katika siku kama ya
leo kikosi cha anga cha utawala ghasibu wa Israel kilifanya shambulizi
la kushtukiza na kuvuka mipaka ya nchi tatu za Misri, Syria na Jordan na
kufanya uharibifu mkubwa. Baada ya shambulizi hilo, vikosi vya nchi
kavu vya Israel vikiwa na silaha za kisasa na uungaji mkono wa Marekani
na Uingereza, vilifanikiwa kuyashinda majeshi ya Misri, Syria na Jordan
katika kipindi cha siku sita tu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!