Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC amewataja
wanamgambo wa kundi la Boko Haram linalopambana na serikali ya Nigeria
kuwa watenda jinai. Iyad Ameen Madani ameyasema hayo baada ya kukutana
na kufanya mazungumzo na Bashiru Aminou Wali Waziri wa Mambo ya Nchi za
Nje wa Nigeria mjini Jeddah na kusema kuwa, hatua ya kundi la Boko
Haram ya kuwauwa na kuwateka nyara watu wasio na hatia inakinzana na
misingi ya dini ya Kiislamu. Madani amesisitiza kwamba, OIC inatangaza
mshikamano wake na wananchi na serikali ya Nigeria kwenye mapambano
dhidi ya kundi la Boko Haram. Katibu Mkuu wa OIC amesema kuwa, dini ya
Kiislamu hairuhusu kwa namna yoyote ile kuua watu wasio na hatia au
kuwateka nyara watoto. Serikali ya Nigeria imekuwa ikilituhumu kundi la
Boko Haram kwa kuua na kujeruhi maelfu ya watu katika kipindi cha miaka
michache iliyopita. Hapo jana, Umoja wa Ulaya uliliweka kundi la Boko
Haram kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na pia kuliwekwa vikwazo.
Home »
siasa afrika
» JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAM (O.I.C) IMELAANI VITENDO VYA KUNDI LA BOKO HARAM
JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAM (O.I.C) IMELAANI VITENDO VYA KUNDI LA BOKO HARAM
Written By Unknown on Tuesday, 3 June 2014 | Tuesday, June 03, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!