Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » # ROAD TO BRAZIL # HIKI NDICHO KIKOSI CHA UFARANSA KITAKACHO KWENDA BRAZIL KILICHO TAJWA NA COACH DESCHAMPS.

# ROAD TO BRAZIL # HIKI NDICHO KIKOSI CHA UFARANSA KITAKACHO KWENDA BRAZIL KILICHO TAJWA NA COACH DESCHAMPS.

Written By Unknown on Tuesday, 3 June 2014 | Tuesday, June 03, 2014

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps, amemjumuisha mshambuliaji wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Franck Ribery katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23, tayari kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zitaanza rasmi nchini Brazil June 12.
Didier Deschamps, amemjumuisha Franck Ribery, kwenye kikosi chake huku taarifa zikizeleza kwamba mchezaji huyo anakabiliwa na maumivu ya mgongo ambayo aliyapata wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Ufaransa walibanwa mbavu na timu ya taifa ya Paraguay kwa kufungana bao moja kwa moja.
Kocha huyo amesema maamuzi ya kumjumusha Ribery katika kikosi chake yametokana na taarifa njema alizozipokea kwa daktari wa timu ya taifa ya Ufaransa, ambapo amemthibitishia, mchezaji huyo anaendelea vizri na atapona ndani ya juma moja lijalo.
Katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kilichotajwa na Didier Deschamps ni mchezaji mmoja tu, aliyefanyiwa mabadiliko ambaye ni mlinda mlango wa klabu ya Olympique de Marseille Steve Mandanda aliye majeruhi, ambapo nafasi yake inachukuliwa na mlinda mlango wa klabu ya St Etienne Stephane Ruffier.

Kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya Ufaransa kinachokwenda nchini Brazil kupamba katika kundi la tano lenye timu za Honduras, Ecuador pamoja na Uswiz, upande wa makipa ni Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Stephane Ruffier (St Etienne) na Mickael Landreau (Bastia)


Mabeki: 
Mathieu Debuchy (Newcastle United), Lucas Digne (Paris St Germain) Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Bacary Sagna (Arsenal), Mamadou Sakho (Liverpool) na Raphael Varane (Real Madrid)


Viungo: 
Yohan Cabaye (Paris St Germain), Clement Grenier (Olympique Lyon), Blaise Matuidi (Paris St Germain), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle United) na Mathieu Valbuena (Olympique Marseille)


Washambuliaji:
Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (Newcastle United) na Franck Ribery (Bayern Munich).


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi