Rais Barack Obama wa Marekani
amesema kuwa jambo ambalo limekuwa likimsumbua katika kipindi cha
uongozi wake ni kushindwa kupunguza viwango vya vitendo vya kimabavu vya
utumiaji silaha nchini humo, akisema kuwa maafa hayo yanamtia hofu.
Rais Obama amesema suala linalomsumbua kichwa hivi sasa ni kuwa jamii
imeshindwa kuonyesha azma ya kuchukua baadhi ya hatua za kimsingi za
kuziondoa silaha mikononi mwa raia ambao wanaweza kusababisha maafa
makubwa sana.
Barack Obama amesema kuwa Marekani ni
nchi pekee iliyoendelea duniani ambayo inakabiliwa na vitendo hivyo vya
mabavu vya utumiaji silaha na kwamba matukio hayo yamekuwa yakitokea
nchini humo mara moja kwa wiki. Obama amesema hakuna sehemu nyingine
yoyote duniani panapojiri vitendo kama hivyo zaidi ya Marekani. Rais
Barack Obama ameyasema hayo masaa machache baada ya mwanaume mmoja
aliyekuwa na silaha kumuua mwanafunzi katika shule moja ya elimu ya juu
huko Oregon.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!