Mpwa wake kocha wa timu
ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amefariki duniani jana kwa ajali
ya gari ikiwa ni siku kabla ya michuano ya Kombe la Dunia. Kwa mujibu
wa taarifa za polisi Tarcisio Joao Schneider mwenye umri wa miaka 48
alipata ajali hiyo karibu na mji wa Passo Fundo ambako ndiko nyumbani
kwa Scolari. Huo ni msiba wa pili kwa kocha huyo katika wiki za hivi
karibuni baada ya kuhudhuria msiba wa kaka yake wa kambo Mei mwaka
huu. Scolari mwenye umri wa miaka 65 ambaye alishinda Kombe la Dunia
akiwa na Brazil mwaka 2002, anatarajiwa kuingoza tena nchi hiyo katika
michuano hiyo katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa jijini Sao Paulo
kesho. Mbali na kuifundisha Brazil kwa vipindi viwili tofauti, Scolari
pia amewahi kuifundisha Ureno, Chelsea, Bunyodkor na Palmeiras.
Home »
michezo ulaya
» KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL AANZA KOMBE LA DUNIA KWA MAJONZI,AMEFIWA NA MPWAE!!!
KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL AANZA KOMBE LA DUNIA KWA MAJONZI,AMEFIWA NA MPWAE!!!
Written By Unknown on Wednesday, 11 June 2014 | Wednesday, June 11, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!