Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » #ROAD TO BRAZIL# KOCHA WA UHISPANIA AWAJIBU WALE WANAOSEMA KUWA MWAKAA HUU HATOWEZA KUTETEA TAJI LA KOMBE LA DUNIA KISA ETI KUMUACHA D.COSTA

#ROAD TO BRAZIL# KOCHA WA UHISPANIA AWAJIBU WALE WANAOSEMA KUWA MWAKAA HUU HATOWEZA KUTETEA TAJI LA KOMBE LA DUNIA KISA ETI KUMUACHA D.COSTA

Written By Unknown on Wednesday, 4 June 2014 | Wednesday, June 04, 2014

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente Del Bosque amekanusha kuwa nafasi ya kikosi chake kutetea taji la Kombe la Dunia itaingia dosari kama Diego Costa hatakuwa fiti. Kocha huyo aliamua kubahatisha kwa kumjumuisha nyota huyo wa Atletico Madrid katika kikosi chake cha mwisho pamoja na mshambuliaji mwenye umri wa miaka 25 kuwa majeruhi aliyopata katika kipindi cha mwisho cha msimu.
Del Bosque anetegemea Costa ambaye alifunga mabao 36 katika mashindano yote msimu uliopita akiwa na klabu yake, kiongozi katika safu ya ushambuliaji mbele ya Fernando Torres na David Villa. Ingawa anapona taratibu nyota huyo mzaliwa wa Brazil ameanza kufanya mazoezi kama kawaida na kikosi cha nchi hiyo Jumatatu kuelekea katika mchezo wao wa mwisho wa kirafiki kabla ya Kombe la Dunia. Akihojiwa kuhusiana na hilo Del Bosque amesema watu wamekuwa wakimuuliza swali hilo wakati wa michuano ya Ulaya mwaka 2012 ambayo walikuwa mabingwa huku wengine wakidai alitumia mfumo usiokuwa na mshambuliaji yaani 4-6-0. Del Bosque amesema ni kweli angependa Costa awemo katika kikosi chake cha mwisho lakini kama hatakuwa fiti kwa asilimia 100 itabidi afanye maamuzi kabla ya kutangaza kikosi cha mwisho, hata hivyo bado anaamini anatakuwa fiti kwa ajili ya michuano hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi