Siku kama ya leo miaka 25
iliyopita, sawa na tarehe 14 Khordad mwaka 1368 kwa mujibu wa kalenda ya
Hijria Shamsia sawa na tarehe 4 Juni 1989 Milaadia, Imam Ruhullah
Musawi Khomeini (M.A) Muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran aliaga
dunia baada ya kuishi kwa miaka 87 katika umri uliojaa juhudi zisizo na
kikomo. Kwa kutangazwa kifo cha Imam ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na
majonzi na huzuni kubwa. Imam Khomeini (M.A) alizaliwa tarehe Mosi
mwezi wa Mehr mwaka 1281 Hijiria Shamsia sawa na tarehe 24 Septemba 1902
Milaadia katika mji wa Khomein ulioko katikati mwa Iran. Alianza
kujishughulisha na siasa sambamba na masuala ya kielimu na kiutamaduni.
Mapambano ya Imam dhidi ya utawala wa Shah na uingiliaji wa Marekani
nchini Iran yalishtadi mwaka 1963 Milaadia sawa na 1342 kwa mujibu wa
kalenda ya Hijria Shamsia, na kupelekea Imam kubaidishwa kwa miaka 13
nchini Iraq, Uturuki na Ufaransa. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata
ushindi mwaka 1357 Hijiria Shamsia sawa na tarehe 1979 Milaadia kwa
uongozi shupavu wa Imam Khomeini (M.A). Aidha Imam alibobea katika elimu
ya dini na mbali na kuwasomesha wanafunzi wengi na kutoa hotuba nyingi
za kihistoria, aliandika pia vitabu. Miongoni mwa vitabu vyake
tunavyoweza kuashiria hapa ni Tahrirul Wasilah, Kashful Asrar, Misbahul
Huda, na Utawala wa Kiislamu na Wilayatul Faqih.
----------------------------------------------------------------
Na Siku kama ya leo miaka 25
iliyopita, sawa na tarehe 4 Juni mwaka 1989, wanafunzi kadhaa wa vyuo
vikuu vya China waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa na polisi katika
mji mkuu wa nchi hiyo Beijing. Siku hiyo maelefu ya wanafunzi wa vyuo
vikuu vya China walikuwa wamekusanyika katika mzunguko wa Tiananmen
mjini Beijing, wenye maana ya 'Amani ya Mbinguni' wakitaka kuwepo
mazingira ya wazi ya kisiasa nchini humo, kupungua uwezo wa chama cha
kisoshalisti, kuongezwa uwezo wa bunge na kuchaguliwa wawakilishi wake.
Ingawa serikali ya China ilipiga marufuku maandamano hayo lakini
wanafunzi waliendela kukusanyika na mwishowe askari polisi na vikosi vya
jeshi vikatumia silaha kuwakandamiza wanafunzi hao.
-------------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 25
iliyopita inayosadifiana na tarehe 4 Khordad mwaka 1368 kwa mujibu wa
kalenda ya Kiirani, Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi
Muadhamu walimchagua Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kuwa Kiongozi
Muadhamu wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Uchaguzi huo
ulifanyika masaa machache tu baada ya kufariki dunia Imam Khomeini (M.A)
ambapo wasia wa Imam ulisomwa pia mbele ya hadhirina. Hadi sasa
Ayatullah Khamenei anaendeleza njia ya Imam Khomeini MA kwa msingi wa
mafundisho ya Kiislamu na ameyaongoza Mapinduzi ya Kiislamu kwa hekima,
tadbiri, uono wa mbali na ustahiki.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!