Kocha wa zamani wa timu
ya taifa ya Misri, Hassan Shehata amebainisha kuwa amefikia makubaliano
na klabu ya Difaa Hassani d'El Jadida ya Morocco kwa ajili ya
kuifundisha msimu ujao. Difaa ilishindwa kumuongeza mkataba kocha wake
Abdelhak Benchikha raia wa Algeria ambaye amechukuliwa na mahasimu wao
Raja Casablanca. Shehata aliuambia mtandao wa Supersport kuwa tayari
wameshafikia makubaliano ya kuingoza timu hiyo kwa misimu miwili na
anachosubiri ni mwenyekiti wa Difaa kwenda jijini Cairo kwa ajili ya
kusaini mkataba na baadae kuutangaza. Taarifa zimekuja sambamba na
taarifa zingine kutoka katika vyombo vya habari kutoka Misri vilivyodai
anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa Zamalek ambayo imetimua kocha wake wa
sasa Ahmed Hossam Mido mwishoni mwa msimu huu. Baada ya kuondoka Zamalek
mwaka 2012, Shehata mwenye umri wa miaka 64 alikwenda kuifundish Al
Arabi ya Qatar kwa miezi michache kabla ya kujiuzulu wadhfa wake huo.
Home »
michezo africa
» KOCHA WA ZAMANI WA MISRI HASSAN SHEHATA AMEPATA ZAKE DILI LAKUINOA KLABU YA DIFAA YA HUKO MOROCCO.
KOCHA WA ZAMANI WA MISRI HASSAN SHEHATA AMEPATA ZAKE DILI LAKUINOA KLABU YA DIFAA YA HUKO MOROCCO.
Written By Unknown on Wednesday, 4 June 2014 | Wednesday, June 04, 2014
Labels:
michezo africa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!