Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imedokeza kuwa inapanga
kumteua balozi atakayeiwakilisha Washington nchini Somalia. Habari
zinasema kuwa, Rais Obama atatangaza balozi wake mpya mjini Mogadishu
hivi karibuni. Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Marekani kuwa na balozi
nchini Somalia tangu kupinduliwa dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Siad
Barre. Marekani ingawa haijawahi kutangaza rasmi kukata uhusiano wa
kidiplomasia na Somalia lakini ilifunga ubalozi wake mjini Mogadishu
mwaka 1991. Serikali ya sasa nchini Somalia ilitambuliwa rasmi na
Marekani mwaka 2013.
Washington ina kumbukumbu chungu ya Somalia kwani mwaka 1993 takriban wanajeshi wake 20 waliuawa na wengine kadhaa wakashikwa mateka baada ya ndege mbili za kijeshi aina ya Black Hawk kutunguliwa na wapiganaji waliokuwa wakiongozwa na mbabe wa zamani wa kivita, Mohamed Farah Aideed. Miili ya wanajeshi hao wa marekani ilizungushwa katika barabara za Mogadishu ikiburutiwa chini. Tukio hilo liliiletea Washington aibu kubwa kimataifa. Wachambuzi wengi wanaamini kuwa, iwapo Marekani itapeleka balozi wake mpya nchini Somalia, hatua hiyo italipa nguvu kundi la wanamgambo wa al-Shabab na yumkini ikapelekea Wasomali kuanza kutoa mashirikiano kwa kundi hilo kwa kuhofia tambia ya Washington ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yao.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!