Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » CHRISTIANO RONALDO AKIWEKA MATATANI KIKOSI KIZIMA CHA URENO BAADA YA AFYA YAKE KUONEKANA KUWA MBAYA.

CHRISTIANO RONALDO AKIWEKA MATATANI KIKOSI KIZIMA CHA URENO BAADA YA AFYA YAKE KUONEKANA KUWA MBAYA.

Written By Unknown on Wednesday, 4 June 2014 | Wednesday, June 04, 2014

Timu ya taifa ya Ureno imeingiwa na mchecheto katika kambi waliyoweka huko New Jersey, Marekani kutokana afya ya mshambuliaji wao nyota Cristiano Ronaldo. Wakati michuano ya Kombe la Dunia ikikaribia, Ronaldo ambaye ni mchezaji bora wa dunia wa mwaka amekuwa na habari mbaya kuhusu maumivu aliyonayo. Chama cha Soka cha nchi hiyo kimetoa taarifa kuwa Ronaldo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya msuli wa nyuma ya mguu wake wa kushoto pamoja na goti katika mguu huo huo. Mbali na Ronaldo wachezaji wengine wa timu hiyo akiwemo Meireles, Pepe na Beto nayo wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha na wote wamekuwa wakifanya mazoezi katika kituo cha mazoezi cha New York Jet ili kuwaweka fiti kabla ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza Juni 12. Wakati Ureno wakiwa wameshazungumzia mara kwa mara juu ya majeraha ya msuli yanayomsumbua Ronaldo hii ni mara ya kwanza kuripoti juu ya maumivu ya goti kwa mchezaji huyo. Ureno imepangwa katika kundi G na watafungua dimba kwa kuikabili Ujerumani Juni 16 huko Salvador kabla ya kuivaa Marekani wiki moja baadae huko Manaus na baadae kumaliza na Ghana katika mechi zake za makundi Juni 26 jijini Brasilia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi