Serikali ya Uingereza imewaonya tena raia wake walioko nchini
Kenya ikisema bado kuna uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi
nchini humo. London imetaja miji ya Mombasa, Wajir, Garissa na Mandera
kuwa maeneo yenye hatari zaidi. Tahadhari hiyo imepuuzwa na maafisa wa
serikali ya Kenya ambao wamesema hatua za kimsingi zimechukuliwa
kuimarisha usalama na kwamba taifa hilo ni salama kwa watalii wa kigeni
na kwa Wakenya kwa ujumla. Wiki chache zilizopita, Uingereza na nchi
zingine za Ulaya zilitoa tahadhari kama hiyo na kupelekea idadi kubwa ya
watalii kuondoka Kenya mara moja. Serikali ya Kenya imelaani hatua hiyo
na kusema Wamagharibi si marafiki wa dhati.
Huku hayo yakijiri, Bunge la Kenya linajiandaa kujadili hoja ya kumfuta kazi mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Bw Isaac Hassa pamoja na makamishna wengine 8 wa tume hiyo. Spika wa bunge hilo, Justin Muturi ameagiza kamati ya bunge ya masuala ya sheria kupitia hoja hiyo iliyowasilishwa na mbunge, Wafula Buke, kabla ya kuanza kujadiliwa bungeni. IEBC inatuhumiwa kuendesha uchaguzi mkuu uliopita kwa njia isiyo ya kitaalamu ambayo imesababisha wanasiasa wengi kupokonywa nyadhifa zao mahakamani kutokana na utata na makosa yaliyojitokeza wakati wa kuchaguliwa kwao.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!