Siku kama ya leo miaka 7 iliyopita, alifariki dunia Ayatullahil-Udhma
Sheikh Muhammad Fadhil Lankarani aalim na marjaa mkubwa wa Kiislamu
baada ya kuugua. Allamah Fadhil Lankarani alizaliwa mwaka 1310 Hijria
Shamsia katika mji wa kidini wa Qum huko kusini mwa Tehran na kuanza
kujifunza masomo ya dini akiwa kijana mdogo. Aidha alipata kustafidi na
mafunzo ya walimu wakubwa wa zama zake kama vile Ayatullahil udhma
Burujerdi na Imam Khomeini Mwenyezi Mungu awarehemu. Ayatullahil Udhma
Sheikh Muhammad Fadhil Lankarani katika kipindi kifupi aliweza kufikia
daraja ya ijtihad.
Siku kama ya leo miaka 51 iliyopita sawa na tarehe 16 Juni 1963,
Valentina Tereshkova mwanamke wa kwanza duniani kwenda angani kutoka
Russia alianza safari yake ya angani kwa kutumia safina ya anga
iliyoitwa Vostok-6. Mwanake huyo alitua katika orbiti ya ardhi wakati
ambapo Valery Bykovsky mwanaanga mwingine wa Russia alipokuwa akizunguka
mzunguko wa dunia. Valentina Tereshkova ambaye alielekea angani miaka
miwili baada ya Yuri Gagarin mwanaume wa kwanza kwenda angani,
alizunguka sayari ya dunia mara 48 kwa muda wa masaa 70 na dakika
hamsini.
Na miaka 70 iliyopita katika siku kama ya leo inayosadifiana na
tarehe 16 Juni mwaka 1944 ikiwa ni wakati wa Vita vya Pili vya Dunia,
wanajeshi wa majini wa Marekani waliaza kushambulia miji ya Japan kwa
kuulenga mji wa Fokula ulioko kusini mwa nchi hiyo kwa mabomu.
Mashambulizi hayo yalipelekea kuuawa makumi ya maelfu ya raia wa Japan
na kuharibiwa viwanda na mashamba ya nchi hiyo. Vita hivyo vilipelekea
Marekani kushambulia kwa mabomu ya nyuklia miji miwili ya Japan ya
Hiroshima na Nagasaki mwezi Oktoba mwaka 1945.
*****************************************
******************************************
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!