Viongozi wa soka barani
Ulaya wamemtaka rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter
kutogombea kwa kipindi kingine kwasababu ya tuhuma za rushwa
zinazoliandama shirikisho hilo. Ofisa Mkuu wa Chama cha Soka cha
Uholanzi Michael Van Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter, FIFA
imeandamwa na tuhuma za rushwa na ili ijisafishe ni sharti Blatter
angatuke. Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Soka Uingereza , Greg
Dyke,ameshtumu kauli ya Blatter kuwa madai ya rushwa kuhusiana na
kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022
yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na ubaguzi wa
rangi. Blatter anatarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania nafasi kipindi
cha tano kuingoza FIFA katika uchaguzi wa shirikisho hilo unaotarajiwa
kufanyika mwaka ujao. Kwa sasa wajumbe wa FIFA wana vikao huko Sao Paulo
wakijiandaa kwa ufunguzi wa Kombe la Dunia hapo kesho ambako Sepp
Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya wale wanaoisema
vibaya FIFA na Qatar.
Home »
michezo ulaya
» MKUU WA FIFA BLATTER AKIONA CHA MOTO AANDAMWA HADI TUMBO KUUMAA,WAMUOMBA ASIJARIBU KUGOMBEA TENA KWENYE WADHIFA HUO
MKUU WA FIFA BLATTER AKIONA CHA MOTO AANDAMWA HADI TUMBO KUUMAA,WAMUOMBA ASIJARIBU KUGOMBEA TENA KWENYE WADHIFA HUO
Written By Unknown on Wednesday, 11 June 2014 | Wednesday, June 11, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!