Home »
siasa kimataifa
» SERIKALI YA KUWAIT YAKABWA KOO NA MAELFU YA WAFUASI WA UPINZANI KISA UFISADI.
SERIKALI YA KUWAIT YAKABWA KOO NA MAELFU YA WAFUASI WA UPINZANI KISA UFISADI.
Maelfu ya wafuasi wa upinzani wanaopinga serikali wameandamana
nchini Kuwait, kutaka kuhitimishwa ufisadi wa mamilioni ya dola
unaodaiwa kufanywa na maafisa wa serikali. Maadamano hayo yamefanyika
kufuatia wito uliotolewa na kiongozi mkuu wa upinzani Musallam al Barrak
ambaye ametishia kutaja majina ya maafisa wanaohusika katika ulaji
rushwa. Akihutubia maandamano hayo Al Barrak ambaye ni mbunge wa zamani
amesema, ufisadi na ulaji rushwa vimeenea katika taasisi zote za nchi,
na kwamba wananchi wanaojitokeza kuhoji suala hilo wanahongwa mamilioni
ya dinar. Kiongozi huyo wa upinzani wa Kuwait amesema kuwa, wamechoshwa
na tatizo hilo na sasa wakati umewadia wa kupambana na ufisadi.
Hayo yanajiri huku utawala wa Kuwait ukijaribu kujitanzua na
kutapakaa sauti za mazungumzo yanayodhihirisha kuwa maafisa wa zamani wa
serikali wanapanga njama dhidi ya utawala wa Kuwait City na Amir wa
nchi hiyo Sheikh Sabah al Ahmed al Sabah. Kadhia hiyo imezusha mjadala
mkubwa nchini humo ambapo serikali imeamuru kufungiwa vyombo vya habari
huku kesi hiyo ikiupa fursa upinzani kwa mara nyingine kupaza sauti
baada ya kutulia kwa karibu mwaka mmoja.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!