Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » MWANAMUZIKI D-BANJ WA NIGERIA AMEKANA HADHARANI UVUMI WA KUWA ANA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MUIGIZAJI WA NOLLYWOOD GENEVIEVE.

MWANAMUZIKI D-BANJ WA NIGERIA AMEKANA HADHARANI UVUMI WA KUWA ANA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MUIGIZAJI WA NOLLYWOOD GENEVIEVE.

Written By Unknown on Monday, 16 June 2014 | Monday, June 16, 2014

Wengi wanaamini kuwa D.Banj aliwahi kukiri kwenye nyimbo zake kuwa anampenda muigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji na hata watu wa karibu wa Genevieve walikaririwa hivi karibuni wakisema kuwa wawili hao ni wapenzi.
D-Banj amekana wazi kuwa na uhusiano na muigizaji huyo katika mahojiano aliyofanya na Vanguard.
“Kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusu mambo mengi. Sipendi kabisa kuzungumzia uhusiano wangu binafsi kwa sababu siku zote watu wananielewa tofauti. Lakini daima tetesi zitabaki kuwa tetesi.”
“Kwa kweli sina uhusiano wa mapenzi na Geneveive. Ngoja niweke mambo sawa.” Amesema DBanj.
Alipoulizwa kama waliwahi kuwa na ukaribu na kutaka kuwa wapenzi alidai yeye binafsi hajawahi kufikia huko.
D.Banj ambaye hivi sasa amefikisha umri wa miaka 34 aliulizwa kuhusu mpango wa kuoa na kutulia na familia na hapo majibu yake yalikuwa tata.
“Ofcourse, ninawaza kuhusu kutulia. Nani kasema sijafunga ndoa? Maisha yangu binafsi lazima yabaki kuwa faragha, hususani kwa vyombo vya habari.”
Ndipo muuliza maswali alipouliza, “Inamaana kuwa DBanj alifunga ndoa kwa siri?”
Dbanj akajibu, “Inaweza kuwa hivyo.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi