Duru za usalama na mahakama nchini Misri zimetangaza kuwa, jeshi la
usalama la nchi hiyo limefunga maduka makubwa yanayomilikiwa na shakhsia
wawili wenye mafungamano na harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchi hiyo.
Tume inayojishughulisha na kuchunguza mali za wanachama wa Ikhwanul
Muslimin imesema kuwa, maduka hayo yaliyofungwa ni pamoja na yale
yanayofahamika kwa jina la Zad yanayomilikiwa na Khairat el-Shater na
yale yanayofahamika kwa jina la Sudi yanayomilikiwa na Abdurahman
as-Sudi.
Kwa mujibu wa idara hiyo inayofuatilia mali za harakati hiyo iliyopigwa marufuku nchini Misri, hatua hiyo imechukuliwa kutekeleza sheria iliyotolewa na serikali ya kuzuia mali zote za wanachama wa harakati hiyo. Kwengineko Ibrahim Mahlab, Waziri Mkuu wa serikali ya muda ya Misri, anatazamiwa kuapishwa leo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo mbele ya Abdel Fattah el-Sisi rais mpya wa Misri. Mahlab amenukuliwa akisema kuwa, tayari mazungumzo na vikao kwa ajili ya kuunda serikali, vimemalizika.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!