Msemaji wa Bi.Catherine Ashton, Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya amesema kuwa, shambulio dhidi ya ubalozi huo mjini Kiev halikubaliki na hivyo amewataka viongozi wa Ukraine kutekeleza ahadi zao kwa mujibu wa makubaliano ya Geneva.
Inaelezwa kuwa, katika machafuko yaliyojiri siku ya Jumamosi karibu na ubalozi wa Urusi mjini Kiev, Ukraine askari wanaotajwa kuwa na mahusiano na serikali waliuzingira ubalozi huo sambamba na kuharibu magari ya ubalozi. Mvutano kati ya Ukraine na Russia unazidi kushika kasi licha ya marais wa nchi hizo kukutana hivi karibuni huko Paris na kuahidiana kuimarisha uhusiano wao. Hapo juzi wanajeshi wenye mafungamano na Russia huko Ukraine waliitungua ndege ya kijeshi katika mji wa Luhansk unaopatikana mashariki mwa Ukraine. Russia iinaitaka Ukraine kusimamisha oparesheni zake za kijeshi katika mikoa ya mashariki mwa nchi na kuanza mazungumzo ya kitaifa ili kukomesha umwagaji damu nchini humo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!