Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » NAIMANI HATA NA WEWE HII ITAKUTIA UCHUNGU,DADA HUYU KAPIGWA HADI AKAWA KIPOFU KISA ETI ANAHISIWA KUWA ANAUHUSIANO NA MWANAUME MWISLAM.

NAIMANI HATA NA WEWE HII ITAKUTIA UCHUNGU,DADA HUYU KAPIGWA HADI AKAWA KIPOFU KISA ETI ANAHISIWA KUWA ANAUHUSIANO NA MWANAUME MWISLAM.

Written By Unknown on Wednesday, 11 June 2014 | Wednesday, June 11, 2014

Ubaguzi wa aina yoyote ni vyema ukapigwa vita mapema kwa kuwa madhara yake ni makubwa kuanzia ngazi ya familia.
Mwanamke mmoja alitajwa kwa jina la Jageer Mirgind wa Uingereza, amepigwa vibaya na kusababishiwa upofu na baba yake wa kambo baada ya kuhisi kuwa ana uhusiano wa mapenzi na kijana wa imani ya kiislamu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Jageer kuhusu tukio hilo yaliyosomwa katika mahakama moja nchini Uingereza, baba yake huyo wa kambo aliyetambulika kwa jina la Manjt Mirgind mwenye umri wa miaka 51 alimvamia na kumburuza hadi jikoni huku akimtishia maisha ‘nitakuua’.

Wakati mzee huyo akitekeleza tukio hilo la kinyama, alikuwepo mtoto wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita ambaye alishuhudia akilia kwa sauti huku akijaribu kumvuta ili asiendelee kumtesa Jageer. Hata hivyo msaada wake haukuwekana. Mzee aliingiza vidole machoni mwa binti yake huyo na kumtoboa macho.
 Mtandao wa Dailymail umeripoti kuwa mzee huyo alichanganywa na simu zilizokuwa zinapigwa kwa watu kwa lengo la kuwatania (prank calls) ili kurusha kwenye vipindi kama sehemu ya show.
Baada ya kusomewa mashitaka yote na kukiri kosa mahakamani, mzee huyo alijitetea kupitia maelezo yaliyosomwa na mwanasheria wake.

“Mimi ni baba wa familia anaefanya kazi kwa bidii ambaye aliacha kazi ili amuangalie/amtunze mama yake aliyekuwa mgonjwa miaka saba iliyopita. Nilikuwa na msogo wa mawazo wakati huo na hakuna kinachoweza kuwa kisingizio kwa kile nilichofanya. Nilikuwa najaribu kumtetea binti yangu. Mimi ni mwanaume ninaependa amani na mwaminifu na najua sitakuwa na nafasi ya kuomba radhi lakini naitumia mahakama kiasi gani naomba radhi.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi