Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » PASINA SABABU YEYOTE KUTAJWA WAKUU WA JESHI KUTOKA MALAWI WAFUTWA KAZI NA RAIS MPYA WA NCHI HIYO.

PASINA SABABU YEYOTE KUTAJWA WAKUU WA JESHI KUTOKA MALAWI WAFUTWA KAZI NA RAIS MPYA WA NCHI HIYO.

Written By Unknown on Thursday, 26 June 2014 | Thursday, June 26, 2014

Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika amewafuta kazi wakuu wa jeshi pasina kutaja sababu yoyote. Taarifa kutoka Ofisi ya Rais imesema kamanda mkuu wa jeshi Jenerali Henry Odillo na naibu wake Meja Jenerali John Msonthi wameondolewa katika nafasi zao.
Peter Mutharika kwa Mbele.
Odillo na Msonthi ambao wote pia waliwahi kuwa wanadiplomasia, wanahusishwa na mgogoro wa kikatiba ulioibuka Aprili 2012 baada ya kifo cha ghafla cha Rais Bingu wa Mutharika. Wakati Bingu alipoaga dunia ilitazamiwa kaka yake, Peter, ambaye wakati huo alikuwa waziri wa mambo ya nje, angechukua kiti cha urais badala ya Joyce Banda ambaye kikatiba alitakiwa achukue nafasi hiyo lakini alikuwa amejiondoa kwenye chama tawala. Katika kizazaa hicho Joyce Banda alikutana na Odillo ambaye alimpa ulinzi kamili na kutangaza kuunga mkono urais wake. Kufuatia uungaji mkono wa jeshi, Banda alitawala hadi Mei mwaka huu wakati uchaguzi wa rais ulipofanyika na Peter Mutharika kuibuka mshindi licha ya kuwepo madai ya wizi wa kura.
Jeshi la Malawi pia limehusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo imepewa jina la 'Cashgate' ambapo mamilioni ya dola ya fedha za umma yalipotea mwaka jana.



TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi