Polisi ya Kenya imemtia mbaroni Gavana wa Kaunti ya Lamu
iliyokumbwa na machafuko hivi majuzi na kusababisha vifo vya watu zaidi
ya 65. Polisi walimshika Issa Timamy, kufuatia tuhuma za kuhusika na
mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni mapema mwezi huu. Inaripotiwa kuwa
kabla ya kukamatwa, Gavana huyo wa Lamu aliitwa na polisi kutoa maelezo
juu ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni katika eneo la Mpeketoni.
Bwana Timamy ni gavana wa pekee kutoka chama cha UDF na anatarajiwa
kupandishwa kizimbani mjini Mombasa ili kujibu mashtaka yanayomkabili.
Itakumbukwa kuwa watu wasiopungua 65 waliuawa katika eneo hilo la Lamu baada ya watu wasiojulikana kufyatua ovyo risasi na kuwalenga watu barabarani na hotelini.
Issa Timamy |
Itakumbukwa kuwa watu wasiopungua 65 waliuawa katika eneo hilo la Lamu baada ya watu wasiojulikana kufyatua ovyo risasi na kuwalenga watu barabarani na hotelini.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!