Wake wa wanasiasa mashuhuri nchini Niger wamekamatwa baada ya kusambaratishwa mtandao wa usafirishaji haramu watoto.
Zaidi ya washukiwa 20 walikamatwa Jumatatu iliyopita kama sehemu ya uchunguzi wa kimataifa uliowahusisha maafisa wa polisi kutoka Nigeria, Benin na Niger.
Kati ya waliokamatwa ni mke wa waziri mkuu wa zamani wa Niger ambaye
hivi sasa ni Spika wa Bunge Hama Amadou anayetajwa kuwa mshindani mkuu
wa Rais Mahamadou Issoufou katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka
2016. Mke wa Waziri wa Kilimo Abdou Labo pia amekamatwa. Watoto
waliosafirishwa kwa njia haramu wanaaminika kuwa waliwasili Niger
wakitokea Benin kwa kupitia Nigeria. Duru zinaarifu kuwa watoto hao
hununuliwa na wanandoa wasio na uwezo wa kupata watoto.
Katika nchi jirani ya Nigeria serikali iliwahi kugundua 'Viwanda vya Watoto' ambapo wasichana wenye umri mdogo hulazimishwa kupata mimba na kisha kuwauza watoto wanaowazaa. Inaarifiwa kuwa watoto waliozaliwa huuzwa kwa maelfu ya dola huku waliowazaa wakipata takribani dola 200. Usafirishaji haramu watoto ndio jinai ya tatu kwa umashuhuri nchini Nigeria baada ya utapeli na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Zaidi ya washukiwa 20 walikamatwa Jumatatu iliyopita kama sehemu ya uchunguzi wa kimataifa uliowahusisha maafisa wa polisi kutoka Nigeria, Benin na Niger.
Hawa watoto walio zaliwa Lagos Nigeria. |
Katika nchi jirani ya Nigeria serikali iliwahi kugundua 'Viwanda vya Watoto' ambapo wasichana wenye umri mdogo hulazimishwa kupata mimba na kisha kuwauza watoto wanaowazaa. Inaarifiwa kuwa watoto waliozaliwa huuzwa kwa maelfu ya dola huku waliowazaa wakipata takribani dola 200. Usafirishaji haramu watoto ndio jinai ya tatu kwa umashuhuri nchini Nigeria baada ya utapeli na ulanguzi wa dawa za kulevya.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!