Mahakama ya juu zaidi nchini Malaysia imelikataa ombi la kanisa
katoliki nchini humo kubadili msimamo wake ili liweze kutumia neno
‘Allah’ kumaanisha Mungu kwa lugha ya kiarabu.
Hata hivyo baada ya mahakama hiyo kutoa amri yake, serikali ya nchi hiyo ilitoa tamko lake kwa vyombo vya habari Jumatatu wiki hii ikieleza kuwa amri hiyo ya mahakama itatumika tu kwenye magazeti ya kanisa katoliki, lakini ni rukhsa kanisani.
Imeeleza kuwa amri hiyo ya mahakama inahusu sheria ya nchi hiyo ya mwaka 2007 inayokataza matumizi ya neno ‘Allah’ yaani Mungu kwenye magazeti.
“Malaysia ni nchi ya dini nyingi na ni muhimu kwamba tumeneji tofauti zetu kwa amani, kwa kufuata sheria na kupitia mazungumzo, heshima kwa pande zote na utulivu.” Lilieleza tamko hilo la serikali.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!