Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mfumo wa rada ya
kisasa na yenye uwezo mkubwa ijulikanayo kama Qader. Mfumo wa Rada ya
Qader umezinduliwa na kuanza kutekeleza oparesheni leo asubuhi katika
sherehe iliyohudhuriwa na Brigedia Jenerali Farzad Esmaili kamanda wa
Kambi ya Jeshi la Anga la Iran ya Khatamul Anbiya (SAW). Rada ya Qader
ina uwezo wa kutekeleza oparesheni katika eneo lenye upana wa kilomita
1100 na umbali wa juu wa kilomita 300. Rada hiyo iliwahi kufanyiwa
majaribio huko nyuma na sasa imewekwa katika maeneo mabli mbali ya Iran
kulinda anga ya Jamhuri ya Kiislamu.
Radar mpya ya Iran |
Jarida la kijeshi la Kizayuni la 'Israel Defense' limekiri
kuwa ustawi wa kiteknolojia na kijeshi wa Iran ni mkubwa zaidi kuliko
nchi za Magharibi zinavyodhani. Jarida hilo limeandika kuwa Rada ya
Qader ni ya kisasa kabisa na kwamba ni thibitisho la uwezo mkubwa wa
Iran katika teknolojia ya kijeshi. Rada ya Qader imetengenezwa katika
Kituo cha Jihadi ya Kujitegemea ya Kitengo cha Anga za Mbali cha Jeshi
la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Rada hiyo ina uwezo wa
kuainisha maeneo ya kulengwa angani mbali na kutambua ndege za adui
ambazo hazionekani kwenye rada nyinginezo. Aidha inaweza kutambua maeneo
yanakorushwa makombora ya cruise na balistiki. Hali kadhalika rada hiyo
inaweza kutambua satalaiti zilizo katika anga za karibu na ina uwezo wa
kufanya kazi katika mazingira yote ya hali ya hewa na uwezo wa
kukabiliana na adui katika vita vya kielektroniki.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!