Home »
siasa afrika
» SERIKALI YA MISRI YAONESHA MOYO WA HURUMA KWA WAZIRI WA ZAMANI KWA KUMFUTIA KESI YA UFISAD.I ILIYO KUWA INAMKABILI
SERIKALI YA MISRI YAONESHA MOYO WA HURUMA KWA WAZIRI WA ZAMANI KWA KUMFUTIA KESI YA UFISAD.I ILIYO KUWA INAMKABILI
|
Habib
al-Adly |
Mahakama moja nchini Misri imemfutia mashtaka ya ufisadi Waziri
wa zamani wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo. Miaka mitatu iliyopita, Habib
al-Adly alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya
kupatikana na hatia ya wizi wa mali ya umma, utumiaji mbaya wa madaraka
yake pamoja na vitendo vingine vya ufisadi. Hata hivyo, Waziri huyo wa
zamani ataendelea kubakia jela kwani bado kuna makosa kadhaa
yanayomkabili.
Habib Al-Adly alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa zaidi ya miaka 10
chini ya dikteta wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak aliyepinduliwa na
wananchi mwaka 2011.
Wafuatiliaji wa siasa za Misri wanasema kufutiwa mashtaka maafisa wa
zamani wa ngazi za juu katika serikali ya Hosni Mubarak ni ishara kwamba
utawala huo wa kiimla unaanza kuinuka na kupata nguvu taratibu. Hosni
Mubarak anaendelea kushikiliwa na vyombo vya usalama huku kesi yake
ikiendelea na wachambuzi wengi wanasema yumkini kesi yake ikaisha kwa
kuhukumiwa kifungo kifupi gerezani kutokana na kubadilika mawimbi ya
kisiasa nchini Misri.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!