Raia wa Brazil wamemsamehe Eduardo da Silva, Mbrazili ambaye jana
alitazamiwa kuwa katika kikosi cha Croatia kilichocheza na timu yao
jijini Sao Paolo.
Lakini mbaya wao ameendelea kuwa Diego Costa wa Hispania.
Lakini mbaya wao ameendelea kuwa Diego Costa wa Hispania.
Raia wa hapa wanahoji kitendo cha Costa kukubali
kucheza taifa jingine wakati angeweza kupata nafasi Brazil, wanaona ni
usaliti kama ule ambao Yuda Eskarioti alimfanyia Yesu. Wanaamini kuwa
ni vigumu kwa Eduardo kucheza timu ya taifa ya Brazil, lakini wanaiona
nafasi ya Costa kucheza Brazil.
Hapa Diego akivaliya jezi ya Uhispania |
Kocha wa Brazil, Luiz Fillipe Scolari, aliwahi
kumtamkia Costa kwamba angeweza kupata namba kikosini kama Fred
angeumia, lakini Costa inadaiwa kuwa alikasirishwa na kitendo hicho.
Baadaye pia ilidaiwa kuwa Scolari alikuwa anamtaka
Costa kwa kuwasiliana na baadhi ya wapambe wa klabu yake ya Atletico
Madrid, lakini kocha wa Hispania, Vicent del Bosque alimpigia simu
Costa mwenyewe na hivyo mchezaji akajiona amethaminiwa zaidi.
Hata hivyo, Scolari na raia wengi wa Brazil
niliongea nao katika mazungumzo ya baa na katika kahawa wanahoji
uhalali wa Costa kuchezea Hispania dhidi ya Brazil tena katika ardhi ya
Brazil.
“Costa ni Yuda. Mbrazil kucheza Hispania wakati
hatuna washambuliaji? Costa ni Yuda. Nasema ni Yuda. Nadhani amepewa
pesa nyingi.”
Anasema Dlamini Sergio, kijana muuza jezi na bidhaa nyingine za timu ya taifa ya Brazil zilizo katika duka moja la huko Brazil.
Lakini inadaiwa kuwa mama yake Costa, pamoja na
wazazi wake Eduardo wameapa kuwashangilia watoto wao katika jezi zao za
timu ya taifa wanazochezea, hata kama wakicheza na Brazil.Yuda mwingine anayezungumzwa sana katika mitaa ya
Sao Paulo ni kiungo Thiago Motta wa Italia. Katika mechi ya kirafiki
iliyowahi kufanyika kati ya Italia na Brazil inadaiwa kuwa Motta
alikuwa anazomewa kila akigusa mpira.Nilipowachunguza Wabrazili nimegundua kwamba wana
tatizo moja dogo tu. Kama wanaamini kuwa hauna nafasi ya kucheza katika
kikosi cha timu yao ya taifa huwa hawakuoni adui kama ukichagua
kucheza taifa jingine.
Lakini kama ungeweza kupata namba katika kikosi
chao lakini ukachagua kucheza taifa jingine kama ilivyo kwa Costa na
Motta, basi unaonekana kuwa adui namba moja wa taifa lao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!