Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, makumi ya maelfu ya watoto nchini Italia wanafanyishwa kazi kwa nguvu; jambo linalokiuka sheria za kimataifa.
UNICEF imetoa ripoti inayoonyesha kuwa, takriban watoto 260,000 wanalazimishwa kufanya kazi zinazohatarisha afya na saikolojia zao kwa ujumla nchini Italia. Ripoti hiyo inasema watoto wengi wanaoshurutishwa kufanya kazi za sulubu ni wale walio chini ya umri wa miaka 14.
Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF, watoto hao hufanya kazi kama wahudumu kwenye mabaa na mahoteli, kwenye mashamba na wengine hutumiwa kusambaza makaratasi yenye matangazo ya biashara na hivyo kuwalazimu kutembea masafa marefu au kusimama kwa muda mrefu. Ukiukaji huo wa haki za watoto unafanyika zaidi kusini mwa Italia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!