Straika,Luis Suarez, anafanya mazoezi usiku na mchana
kuhakikisha anapona maumivu ya goti kwa wakati ili kuwahi mechi ya
Kombe la Dunia ambapo kikosi chake cha Uruguay kitashuka uwanjani
kesho Jumamosi kumenyana na Costa Rica.
Staa mwenzake, Cristian Rodriguez, amefichua
kwamba Suarez halali na amekuwa akifanya mazoezi ya nguvu muda wote ili
kuwahi mechi ya kwanza kwenye Kundi D, lakini kocha Oscar Tabarez
alisema bado hafahamu lini mchezaji huyo atakuwa fiti.
“Jamaa halali kabisa, anafanya mazoezi usiku na mchana kuhakikisha anakuwa fiti kwa haraka zaidi,” alisema Rodriguez.
Fowadi huyo wa Liverpool alifanyiwa upasuaji Mei
22 baada ya kuumia mazoezini. Kwa sasa anauguza jeraha na amekuwa
akifanya mazoezi ya kila aina kuhakikisha anaziwahi mechi za makundi
za michuano hiyo.
Baada ya kucheza na Costa Rica, Uruguay itamenyana
na England, Juni 19 kabla ya kumalizia mechi ya mwisho kwenye kundi lao
dhidi ya Italia siku tano baadaye.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!