Taasisi ya kimataifa ya kuchunguza mienendo ya kiuchumi ya FITCH
imetoa ripoti inayoonyesha kuwa, satua ya kiuchumi ya Afrika Kusini
imepungua mno katika miaka ya hivi karibuni kutokana na migomo ya kila
mara ya wafayakazi katika sekta ya madini.
Ripoti ya FITCH inasema kuwa, sarafu ya Rand ya Afrika Kusini imekuwa ikipoteza thamani katika siku za hivi karibuni, jambo linaloonyesha kudorora uchumi wa nchi hiyo. Taasisi hiyo imeashiria migomo katika sekta za madini pamoja na uhaba wa umeme na kusema hali hizo zimesababisha kuporomoka satua ya kiuchumi ya Afrika Kusini.
Mwaka uliopita na mwanzoni mwa mwaka huu, Afrika Kusini imeshuhudia migomo chungu nzima ya wafanyakazi wa migodi ya dhahabu na Platinum ambao wamekuwa wakidai nyongeza ya mishahara yao na kuboreshwa mazingira yao ya kazi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!