Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » KUTANA NA HUYU JAMAA ALIYE MKOPI RONALDINHO KILA KITU YANI STYLE ZOTE NAKWENDA KUVAMIA MAZOWEZI YA ARGENTINA.

KUTANA NA HUYU JAMAA ALIYE MKOPI RONALDINHO KILA KITU YANI STYLE ZOTE NAKWENDA KUVAMIA MAZOWEZI YA ARGENTINA.

Written By Unknown on Friday, 13 June 2014 | Friday, June 13, 2014

Super star wa Argentina,ajulikanae kama Lionel Messi, amebaki kwenye mshangao mkubwa na kuamua kucheka tu alipokuwa mazoezini na kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia keshokutwa Jumapili baada ya kuvamiwa na shabiki mmoja aliyefanana na staa wa Brazil, Ronaldinho.
Messi na wenzake walikuwa wakijifua kuelekea mechi dhidi ya Bosnia, ndipo shabiki huyo aliyefanana sana na Ronaldinho alipoingia uwanjani na kumfuata staa huyo wa Barcelona. Jambo hilo liliwafanya wachezaji wa timu hiyo waangue kicheko kwa mshangao. Hata hivyo, shabiki huyo baadaye alitolewa nje ya uwanja na walinzi waliokuwapo uwanjani hapo kulinda mazoezi ya kikosi hicho.
Shabiki huyo hakuwa peke yake aliyevamia uwanjani, mwingine aliingia na kwenda moja kwa moja kufuta vumbi katika viatu vya staa huyo na mashabiki wengine walikimbilia mpira uliokuwa ukitumika kwenye mazoezi hayo wakitaka kuondoka nao.
Kwa upande mwingine, Argentina ilikumbana na kasheshe pia ya kuzomewa na mashabiki wachache wakati wachezaji wake walipotua kwenye mji wa Belo Horizonte.
Zaidi ya mashabiki 5,000 walihudhuria mazoezi hayo yaliyofanyika uwanjani Belo Horizonte Independencia kutazama mazoezi ya timu hiyo hasa kwa mastaa Messi na Angel Di Maria.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi