Siku kama ya leo miaka 1180 iliyopita yaani tarehe 15 Shaaban mwaka
255 Hijria alizaliwa mwana wa Imam Hassan Askari ambaye ni miongoni mwa
wajukuu watukufu wa Mtume Muhamamd (saw) Mahdi (af) katika mji wa
Samarra nchini Iraq. Miaka mitano ya mwanzoni Mahdi (as) aliishi na baba
yake na kuchukua hatamu za uongozi wa umma wa Kiislamu baada ya kuuawa
shahidi baba yake mtukufu. Tangu wakati huo Imam alitoweka mbele ya
macho ya watu na kwa kipindi cha miaka 69 alikuwa akiwasiliana na umma
kupitia wawakilishi wake makhsusi. Baada ya kipindi hicho ambacho
kinatambuliwa kuwa ni cha 'Ghaiba Ndogo', Imam Mahdi alikwenda kwenye
Ghaiba Kubwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu na atadhihiri tena kuja kuleta
uadilifu, usawa na haki duniani baada ya kujazwa dhulma na uonevu.
Tunamuomba Allah aharakishe kudhihiri kwake.
Siku kama ya leo miaka 31 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 23
Khordad 1362 Hijria Shamsia, Bi. Nusrat Amin, faqihi na mfasiri mkubwa
wa Qurani Tukufu alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 97 katika mji wa
Esfahan ulioko katikati mwa Iran. Bi. Nusrat Amin aliutumia muda wake
wote katika kuishughulikia Qurani Tukufu, na hata kufanikiwa kufasiri
juzuu 15 za Qurani na kuandika vitabu kadhaa kama vile 'Njia ya Kufikia
Saada na Nafahat Ar-Rahmania.
Na Siku kama ya leo miaka 93 iliyopita, inayosadifiana na 13 Juni
1921 katika miaka ya mwanzo ya usimamizi wa Uingereza huko Palestina,
kulianzishwa harakati kubwa katika ardhi yote ya Palestina inayokaliwa
kwa mabavu na maghasibu wa Kizayuni. Harakati hiyo ilikuwa dhidi ya
Wazayuni. Harakati ya wananchi hao ilibainisha upinzani wao dhidi ya
siasa za kikoloni za Uingereza pamoja na uungaji mkono wa nchi hiyo kwa
Wazayuni waliokuwa wameiteka ardhi ya Palestina. Siasa za Kikoloni za
Uingereza zilijumuisha kuwashajiisha Wazayuni kutoka sehemu zote duniani
waelekee Palestina ili kwa mujibu wa Azimio la Balfour, serikali ya
Kizayuni iundwe ndani ya ardhi ya Palestina. Sera hiyo ya kikoloni
ilitekelezwa mwaka 1948 wakati dola bandia la Israel lilipoundwa.
------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!