Siku kama ya leo miaka 1397
iliyopita mwafaka na tarehe 5 Shaaban mwaka 38 Hijria Ali bin al
Hussein, mmoja wa wajukuu wa Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW alizaliwa
katika mji mtakatifu wa Madina. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kutokana
na kuwa pamoja na baba yake yaani Imam Hussein AS mjukuu wa Mtume
Muhammad SAW, mtukufu huyo alipata mafunzo mema ya kimaanawi na kiaklaqi
na kunufaika na mafunzo ya bahari kubwa ya elimu ya baba yake. Mtukufu
Ali bin al Hussein AS alisifika kwa takwa na kumcha Mwenyezi Mungu kwani
alikuwa akikesha usiku kwa ajili ya ibada. Alipewa lakabu ya Sajjad
yaani mtu anayesujudu sana kutokana na sijda zake za muda mrefu
alizokuwa akizifanya kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu SW.
Katika tukio la Ashura ambapo baba yake mtukufu, Imam Hussein AS na
idadi kubwa ya wajukuu wa Mtume SAW waliuawa shahidi, Hadhrat Sajjad AS
hakuweza kushiriki katika Jihad kutokana na ugonjwa mkali. Baada ya
Hamasa ya Karbala, Hadhrat Sajjad akiwa na shangazi yake yaani Bibi
Zainab SA walianza kufichua vitendo vya kidhulma vya Bani Umayya sambamba
na kuarifisha Ahlul Bayt kwa umma. Alichukua uongozi wa Waislamu tokea
wakati huo hadi mwisho wa umri wake uliojaa baraka yaani mwaka 94
Hijria.
-------------------------------------------------------------------
Miaka 512 iliyopita siku kama
ya leo, Vasco da Gama baharia wa Kireno alifanya mauaji ya umati huko
Calicut, mji ambao hivi sasa imepewa jina la Kozhikode, ni bandari
iliyoko huko Madras kusini mwa India. Bandari hiyo ilikuwa eneo la
kwanza alipofikia baharia Vasco da Gama mwaka 1498 Miladia na baadaye
kulikalia kwa mabavu eneo hilo. Vasco da Gama kama walivyo wakoloni
wengine, alidai kuwa mmiliki halisi wa India. Vasco da Gama alitoa amri
ya kukatwa, masikio na pua za mabaharia wa Kiarabu wakati walipowasili
katika bandari ya Calicut kwa jili ya kufanya biashara ya mchele. Pia
aliwauwa kwa umati wafanyabiashara hao wa Kiarabu baada ya kuzichoma
moto meli zao.
--------------------------------------------------------------------
Siku kama ya leo miaka 51
iliyopita, Imam Khomeini (M.A), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
alitoa hotuba kali ya kihistoria dhidi ya utawala wa kitwaguti wa Iran,
kwa mnasaba wa Ashura ya Imam Husseini (A.S). Imam Khomeini alitoa
hotuba hiyo mbele ya hadhara kubwa ya wananchi na wanazuoni katika
Madrasa ya Faidhiya katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran, licha ya
vizuizi na vitisho vya utawala wa Shah. Imam alikosoa vikali usaliti wa
utawala wa Shah na vibaraka wake na kukosoa hiyana ya utawala huo dhidi
ya wananchi Waislamu wa Iran. Sehemu ya hotuba ya Imam Khomeini ilisema
hivi kama ninavyomnukuu: "Watu hao wanapinga Uislamu na wanazuoni na
wana nia ya kuutokomeza. Enyi wananchi, dini yetu ya Kiislamu na nchi
yetu viko hatarini na tuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Iran," mwisho
wa kunukuu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!