Mary Robinson Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
katika masuala ya Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika amesisitiza umuhimu
wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki nchini Burundi. Bi. Mary Robinson
ameyasema hayo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais
Pierre Nkurunziza wa Burundi mjini Bujumbura. Mwakilishi wa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa ametaka ufanyike uchaguzi huru na wa haki mwakani pamoja na kushirikishwa wawakilishi wa mirengo yote ya kisiasa
nchini Burundi. Mary Robinson amesema kuwa, uchaguzi mkuu nchini Burundi
una umuhimu mkubwa kwa jamii ya kimataifa na kusisitiza kwamba
wasimamizi wa kigeni wanapaswa kuhudhuria kabla na wakati wa kufanyika
uchaguzi huo. Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
lilielezea wasiwasi wake kuhusiana na mivutano ya kisiasa iliyoko nchini Burundi na mbinyo wa uhuru wa kiraia na ule wa vyombo vya habari yakiwemo
magazeti.
Home »
siasa afrika
» UCHAGUZI MKUU NCHINI BURUNDI UNA UMUHIMU MKUBWA KWA JAMII YA KIMATAIFA:MARY ROBINSON
UCHAGUZI MKUU NCHINI BURUNDI UNA UMUHIMU MKUBWA KWA JAMII YA KIMATAIFA:MARY ROBINSON
Written By Unknown on Tuesday, 3 June 2014 | Tuesday, June 03, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!