Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » VITENDO VIOVU VYA MAJESHI YA FARDC VINAVYO LINDA AMANI HUKO JAMUHURI YA AFRICA YA KATI VYALAUMIWA NA SHIRIKA LA HRW

VITENDO VIOVU VYA MAJESHI YA FARDC VINAVYO LINDA AMANI HUKO JAMUHURI YA AFRICA YA KATI VYALAUMIWA NA SHIRIKA LA HRW

Written By Unknown on Tuesday, 3 June 2014 | Tuesday, June 03, 2014

Shirika la Kuteta Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekosoa vikali vitendo vilivyofanywa na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaolinda amani Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imewatuhumu wanajeshi wa kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kutenda vitendo visivyolingana na sifa na majukumu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika MISCA huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. 
Shirika la Human Rights Watch limeeleza kuwa, tarehe 24 Machi askari hao wa Kongo waliizingira  na kuwatia mbaroni watu 11 waliokuwa ndani ya nyumba moja ya makazi ya raia, na hadi leo haijulikani hatima ya watu hao. Taarifa hiyo imesema kuwa, wanajeshi wa Kongo wamepelekwa  Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ajili ya kulinda maisha ya wananchi wa nchi hiyo na wala siyo kuwaongezea machungu zaidi wananchi wa nchi hiyo iliyogubika na machafuko. Hata hivyo, kikosi cha MISCA kimeanza kuchunguza tuhuma hizo zilizoelekezwa kwa wanajeshi wa Kongo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wanamgambo wa  Kikristo wa Anti Balaka walianzisha machafuko na mauaji dhidi ya Waislamu mwezi Disemba mwaka jana, yaliyopelekea watu wasiopungua milioni moja kulazimika kuwa wakimbizi  wengi wao wakiwa Waislamu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi