Home »
siasa afrika
» SOMA KILE ALICHO KISEMA RAIS MPYA WA MALAWII BAADA YA KULA KIAPO KAMA RAIS MPYA WA NCHI HIYO.
SOMA KILE ALICHO KISEMA RAIS MPYA WA MALAWII BAADA YA KULA KIAPO KAMA RAIS MPYA WA NCHI HIYO.
Rais Peter Mutharika wa Malawi amesema kuwa, sera za serikali yake
zitajikita zaidi katika kuleta uthabiti wa kiuchumi na umoja wa kitaifa
nchini humo. Akizungumza mara baada ya kuapishwa rasmi jana kuwa Rais wa
Malawi, Peter Mutharika ameongeza kuwa uchumi wa nchi hiyo utastawi
hadi kufikia asilimia saba kwa mwaka. Rais Peter Mutharika ni ndugu wa
Bingu wa Mutharika Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyefariki dunia Aprili
2012 na nafasi yake kuchukuliwa na Makamu wake Joyce Banda ambaye
alishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 20 mwezi
uliopita. Joyce Banda alifeli katika juhudi zake za kuboresha hali ya
uchumi, uhaba wa nishati na hasa mafuta na kuzuia kuporomoka sarafu ya
nchi hiyo.
|
Hapo ndipo akila kiapo hiyo May 31 |
Mfuko wa Kimataifa wa Fedha IMF umeeleza kuwa, tokea Joyce
Banda aliposhika madaraka ya nchi hiyo mwaka 2012, thamani ya sarafu ya
nchi hiyo ilizidi kuporomoka na bei za bidhaa mbalimbali kupanda
maradufu. Mashirika ya kifedha duniani pamoja na nchi wahisani
zilisimamisha kutoa misaada ya kifedha kwa Malawi baada ya kufichuliwa
kashfa ya ufisadi wa mamilioni ya dola katika serikali ya Joyce Banda.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Rais Peter Mutharika aliapishwa rasmi jana
mjini Blantyre, kwenye sherehe ambazo zilisusiwa na washindani wake
kwenye uchaguzi huo ambao ni Bwana Lazarus Chakwera wa Malawi Congress
Party na Joyce Banda Rais aliyeondoka madarakani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!