Kampeni ya kuitaka kuishinikiza serikali ya Nigeria kuongeza
bidii katika kuwarudisha watoto zaidi ya 200 waliotekwa na Boko Haram
iliyopewa jina ‘Bring Back Our Girls’ na wananchi wanaofanya maandano
nchini humo imewekewa kizuizi na jeshi la polisi.
Polisi wamepiga marufuku maandamano hayo katika jiji la Abuja kwa madai kuwa yanazua hatari kwa raia wengine.
Hata hivyo, wiki iliyopita kundi lingine la waandamanaji liliibuka na kauli mbiu tofauti na ile ya ‘Bring Back Our Girls’ iliyosambaa duniani kote likaanzisha ‘Release Our Girls Boko Haram’.
Kundi hilo lilivuruga kwa kiasi fulani kampeni ya awali ya waandamanaji na lilijitetea kuwa limeweka neno ‘Boko Haram’ kwa makusudi kwa kuwa sio serikali yenye watoto hao bali kundi hilo ndilo linahusika.
Kundi la Boko Haram limewashikilia wasichana zaidi ya 200 wa Nigeria tangu April mwaka huu na limeipa serikali ya Nigeria masherti ya kutaka kubadilishana na wafungwa wao wanaoshikiliwa na serikali hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!