Mjumbe mwandamizi wa Kamati ya Afya ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA
amesema kuwa, wachezaji Waislamu watakaofunga mwezi mtukufu wa
Ramadhani, hawataathirika kiafya wakati wa kuendelea michuano ya kombe
la dunia nchini Brazil. Jiri Dvorak amesema kuwa, Kamati ya Afya ya Fifa
imefanya uchunguzi na utafiti wa kina kuhusiana na afya za wachezaji
katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kufikia natija hii kwamba, iwapo
wachezaji Waislamu watakula vyakula vinavyohitajika, hawatadhoofika
kimwili katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Drovak ameongeza kuwa, kamati hiyo imefanya uchunguzi wa kutosha, hivyo hakuna ulazima wowote kwa wachezaji kuingiwa na wasiwasi kutokana na michuano hiyo kuingiliana na mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Wakati huohuo, Michel D'Hooghe Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya FIFA amesema kuwa, hakutakuwa na tatizo lolote kwani utaratibu utakuwa kama ule uliofanyika wakati wa michuano ya Olimpiki iliyofanyika 2012 mjini London, Uingereza. Inatarajiwa kwamba, Waislamu wataanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia siku ya Jumamosi au Jumapili ijayo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!