Siku kama ya leo miaka 171 iliyopita, tanuu za feleji maarufu kwa
jina la tanuu za Bessemer zilivumbuliwa. Mvumbuzi wa tanuu hizo alikuwa
Mwingereza Henry Bessemer. Tanuu hizo zilitumika huko Uingereza kwa mara
ya kwanza na leo hii zinatumika katika masuala mbalimbali viwandani.
*******************************************
Tarehe 24 Juni miaka 202 iliyopita, Caracas mji mkuu wa Venezuela
ulidhibitiwa na Simon Bolivar ikiwa ni wakati wa mapambano ya mpigania
uhuru huyo dhidi ya wakoloni kwa ajili ya kuyakomboa maeneo ya Amerika
ya Kusini. Mkoloni Muhispania alishindwa katika vita hivyo vilivyodumu
kwa kipindi cha chini ya mwaka mmoja na baada ya ushindi huo Simon
Bolivar anayejulikana kama shujaa wa mapambano dhidi ya wakoloni huko
Amerika Kusini, aliasisi Shirikisho la Colombia Kubwa. Shirikisho hilo
lilijumuisha nchi za Venezuela, Colombia, Panama na Ecuador, na Bolivar
alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa shirikisho hilo.
*******************************************
Na miaka 202 iliyopita katika siku kama leo, Napoleone Bonaparte
mtawala wa Ufaransa akiwa na kikosi cha askari 350,000 alianza kufanya
mashambulio dhidi ya utawala wa Russia wa Tsar. Miaka mitano kabla ya
tukio hilo, nchi mbili hizo zilikuwa zimetiliana saini mkataba wa
kutoshambuliana kijeshi. Hata hivyo taratibu uhusiano baina ya tawala
mbili hizo ulianza kuharibika, na hivyo kumfanya Bonaparte afikie hatua
ya kuandaa jeshi kubwa na kuishambulia Russia na kisha kusonga mbele
hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow. Hata hivyo hali mbaya ya hewa
yaani baridi kali na kutowafikia wanajeshi wa Kifaransa vifaa muhimu na
suhula za kivita, kuliwafanya askari hao wakabaliwe na hali ngumu katika
medani ya vita. Askari jeshi wapatao 30,000 wa Kirusi walivishambulia
vikosi vya Bonaparte na kuwaua wengi miongoni mwao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!