Mhubiri maarufu Mwislamu ameuawa katika mji wa Garissa kaskazini
mashariki mwa Kenya. Duru zinaarifu kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad
alipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana Jumapili usiku mjini
Garissa.
Mkuu wa Polisi katika kaunti ya Garissa Charles Kinyua amesema mhubiri huyo alipigwa risasi mara kadhaa kwa karibu mita chache tu kutoka Msikiti wa Khalifa karibu na Hospitali Kuu ya Garissa. Alikuwa amefika msikitini hapo kuswali sala ya Isha. Afisa huyo wa polisi amesema lengo la waliomuua bado halijulikani lakini amesema yamkini kundi la kigaidi la al-Shabab limehusika kwani limewahi kuhusika na hujuma kadhaa za kigaidi mjini hapo. Aidha amedai kuwa mhubiri huyo alikuwa na wapinzani ambao hawakutaka ahubiri katika baadhi ya misikiti. Duru mjini Garissa zinadokeza kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad aliwahi kunusurika shambulizi sawa na hilo wakati alipoviziwa katika hoteli moja mjini humo.
Katika miaka ya hivi karibuni wahubiri kadhaa Waislamu wameuawa nchini Kenya hasa katika mji wa Mombasa.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!