Makumi ya wanachama wa kundi la Boko Haram la nchini Nigeria wameuawa
katika mapigano na vikosi vya usalama vya Cameroon. Kwa mujibu wa redio
ya taifa nchini Cameroon, wapiganaji hao wapatao 40 wa kundi hilo
waliuawa jana katika mapigano makali na jeshi la nchi hiyo yaliyojiri
kaskazini mwa nchi. Mapigano hayo yalitokea huko magharibi mwa mji wa
Kousseri karibu na mpaka wa pamoja wa Cameroon, Nigeria na Chad. Aidha
mapigano hayo yanatajwa kuibuka baada ya wanamgambo wasiojulikana na
wanaodhaniwa kuwa ni wanachama wa kundi hilo, kuwaachilia huru mateka
watatu kutoka Italia na Canada waliokuwa wakishikiliwa katika eneo hilo.
Itakumbubwa kuwa mwanzoni mwa wiki iliyomalizika, serikali ya Yaoundé
inayoongozwa na Rais Paul Biya, ilituma maelfu ya askari maalumu wa
kukabiliana na machafuko walioandamana na magari kadhaa ya deraya katika
mpaka wa pamoja na Nigeria kwa lengo la kukabiliana na wanachama wa
kundi hilo. Kundi la Boko Haram limeshadidisha mashambulizi yake katika
siku za hivi karibuni, kikiwemo kitendo cha utekaji nyara wanafunzi wa
kike wa shule ya kutwa, suala lililozivutia hisia za waliowengi ndani na
nje ya nchi hiyo.
Home »
siasa afrika
» WAPIGANAJI WAPATAO 40 WA KUNDI LA BOKO HARAM LA NIGERIA WAMEUWAWAA NA MAJESHI YA CAMEROON
WAPIGANAJI WAPATAO 40 WA KUNDI LA BOKO HARAM LA NIGERIA WAMEUWAWAA NA MAJESHI YA CAMEROON
Written By Unknown on Monday, 2 June 2014 | Monday, June 02, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!