Maafisa wa afya duniani wanaarifu kuwa watu
wasiopungua 208 wameaga dunia kutokana na virusi vya Ebola nchini Guinea
baada ya ugonjwa huo kusambaa kwa siku za hivi karibuni.
Angaa watu 21 waliaga dunia na visa vingine 37
vinavyohusiana na Ebola kuripotiwa kati ya tarehe 29 mwezi Mei na tarehe
1 mwezi Juni na kufikisha idadi ya visa hivyo kufikia 328 katika taifa
hilo lililoko magharibi mwa Afrika.Kati ya visa hivi, 193 vilithibitishwa kupitia vipimo vya maabara.
Hadi sasa, hakuna dawa za kuzuia wala kutibu Ebola- moja kati ya virusi hatari sana duniani.
Zaidi ya nusu ya vifo vya hivi karibuni vilitokea kusini mwa eneo la Guekedou, mahali ambapo ugonjwa huo ulianzia.
Visa vitatu vimedhibitishwa na vingine 10 vinavyodhaniwa kuwa wa ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi Jirani ya Sierra Leone.
Huyu hapa ni mgonjwa wa Ebola akipokea matibabu |
Hata hivyo, binadamu wana nafasi nzuri ya kupona iwapo ugonjwa huo utatambuliwa mapema na kupata matibabu.
Wataalamu kutoka shirika la afya ulimwenguni pamoja na madaktari wasio na mipaka wanaofanya kazi katika eneo hilo wanachunguzwa baada ya uwezekano wa kuathiriwa na Ebola.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!