Jeshi la Sudan limetangaza kuwa, limefanikiwa kuwaangamiza waasi
110 wa Harakati ya Wananchi katika eneo la al Atmour lililoko katika
jimbo la Kordofan Kusini, kusini mwa Sudan.
Msemaji rasmi wa jeshi la Sudan amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuwashambulia waasi katika eneo hilo ambalo hivi karibuni lilikombolewa kutoka mikononi mwa waasi hao. Al Swawarimi Khalid Saad amesema kuwa, operesheni hiyo ambayo ilifanyika kwa mafanikio makubwa ilichukua muda wa masaa matatu.
Majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile yaliyoko kusini mwa Sudan, yamekumbwa na ghasia na machafuko tokea ilipojitawala serikali ya Sudan Kusini mwaka 2011, na serikali ya Khartoum imekuwa ikiituhumu serikali ya Juba kwa kuunga mkono harakati za makundi ya waasi katika majimbo hayo mawili.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!