Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WAHAMIAJI HARAMU WAPATAO 114 WAMEKAMATWA HUKO LIBYA IKIDAIWA WALIKUWA WAKITOKA AFRICA

WAHAMIAJI HARAMU WAPATAO 114 WAMEKAMATWA HUKO LIBYA IKIDAIWA WALIKUWA WAKITOKA AFRICA

Written By Unknown on Friday, 6 June 2014 | Friday, June 06, 2014

Maafisa wa usalama katika pwani ya Libya wamewakamata wahamiaji haramu 114 kutoka nchi za Kiafrika ambao walikuwa wamejazana ndani ya boti moja ndogo wakielekea bara Ulaya.
Maafisa wa Gadi ya Ulinzi ya Pwani ya Libya walisema jana Alkhamisi kuwa waliwakamata wahajiri hao haramu karibu na eneo la Gharbouli mashariki mwa Tripoli. Imedokezwa kuwa wahajiri hao waliokamatwa ni kutoka nchi za eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika hasa kutoka Senegal. Aghalabu ya wahajiri hao haramu huingia Libya kupitia mipaka ya kusini mwa nchi hiyo ambapo ina mipaka ya pamoja na Sudan, Chad, Nigeri na Algeria. Mwaka huu pekee wahamiaji 43,000 wameingia Italia wakitokea eneo la Kaskazini mwa Afrika hasa Libya. Njia ya Libya inatumiwa na wahamiaji hao kutokana na ghasia zinazoendelea nchini humo ambazo zimepelekea serikali kushindwa kuidhibiti ipasavyo mipaka ya nchi kavu na baharini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi