Shirikisho la soka duniani FIFA, limewapiga marufuku
viongozi wa FC Barcelona kuweka hadharani shughuli zozote zinazohusiana
na usajili wa mshambuliaji kutoka Uruguay, Luis Alberto Suares Diaz,
baada ya kukamilisha usajili wake akitokea kwenye klabu ya Liverpool ya
nchini Uingereza.
FIFA wametangaza marufuku kwa viongozi wa FC Barcelona, baada ya mitandao mbali mbali kuanza kuonyesha jezi za mshambuliaji huyo zenye namba tisa mgongoni ambazo zimeanza kuchapishwa kwa ajili ya kufanyiwa biashara.
FC Barcelona wametakiwa kutokufanya hivyo kufuatia adhabu ya Luis Suarez ya kufungiwa miezi minne ya kutojihusisha na masuala ya soka, kutokana na kaadhia aliyoionyesha wakati wa fainali za kombe la dunia, kwa kumng’ata beki wa timu ya taifa ya Italia Georgia Chiellini.
FC Barcelona walikamilisha uhamisho wa Luis Suarez juma lililopita kwa gharama ya paund milion 75, ikiwa ni sehemu ya mikakati iliyowekwa na meneja mpya wa klabu hiyo ya Cataluña, Luis Enrique ya kukisuka upya kikosi cha Barca.
Hata hivyo Luis Suarez anasubiri rufaa yake kusikilizwa na mahakama ya kimichezo CAS, baada ya kuiwasilisha juma lililopita huku akipnga adhabu iliyotangazwa dhidi yake na kamati ya nidhamu ya FIFA.
Suarez aliamua kuiwasilisha rufaa yake CAS, baada ya kamati ya rufaa ya shirikisho la soka duniani FIFA, kubariki adhabu aliyopewa na kamati ya nidhamu baada ya kubainika alimng’ata kwa makusudi Giorgio Chiellini.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!