Daktari Erik Fosse raia wa Norway ambaye yuko katika eneo la Ukanda wa
Gaza linalozingirwa na utawala wa Israel kwa miaka kadhaa sasa,
ameukosoa vikali utawala huo ghasibu kwa kutupa mabomu yenye kusababisha
maradhi ya saratani dhidi ya wananchi wa Palestina walioko katika eneo
hilo. Daktari Fosse ameongeza kuwa, idadi kubwa ya wagonjwa waliolazwa
kwenye hospitali za Gaza ni raia wa kawaida, watoto wakiunda asilimia 30
ya majeruhi hao. Daktari huyo raia wa Norway aliyeko Gaza ameongeza
kuwa, utawala wa Israel unatumia chombo cha kuripulia kiitwacho Dense
Inert Metal Exploxive 'DIME' ambacho kinasababisha maafa makubwa kwa
watu wanaopatwa na athari za mlipuko huo.
Wataalamu wa masuala ya kijeshi wanasema kuwa, chombo hicho cha mripuko kina minunurisho midogo na yenye kuleta maafa na taathira kubwa za kibiolojia. Daktari Erick Fosse ambaye ni mkuu wa kitengo kimoja cha hospitali katika Chuo Kikuu cha Oslo nchini Norway amesema kuwa, baadhi ya majeruhi wa Kipalestina wamekubwa na majeraha yanayosababishwa na silaha mpya, na kusisitiza kwamba hata madaktari wenye uzoefu katika maeneo ya kivita hawajaweza kugundua sababu za majeraha hayo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika vita vilivyopita, utawala wa Israel ulitumia mabomu ya vishada yenye mada za fosforasi nyeupe na yale yaliyokuwa na urani iliyodhoofishwa dhidi ya wakaazi wa Gaza.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!