Michel Djotodia amechaguliwa tena kuendelea kuuongoza muungano wa
waasi wa zamani wa SELEKA huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wanachama
waandamizi wa kundi hilo kwenye mkutano wao wa hapo jana katika mji wa
Birao ulioko kaskazini mwa CAR walipitisha kwa kauli moja kwamba, Bw.
Djotodia aendelee kuwa kiongozi mkuu wa muungano huo. Jenerali Nurdin
Adam ameteuliwa kuwa naibu kiongozi wa kundi la Seleka.
Kundi la Seleka mwaka 2012 lilipigana na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyokuwa ikiongozwa na Rais Francois Bozize ambapo mwezi Machi mwaka uliopita kundi hilo lilifanikiwa kuipindua serikali ya Bozize. Mkuu wa Seleka, Michel Djotodia, alijitangaza kuwa rais wa nchi hiyo baada ya mapinduzi hayo lakini naye akalazimishwa kujiuzulu na viongozi wa jumuiya ya ECCAS mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kushindwa kudhibiti hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa sasa kundi la Seleka bado linahesabiwa kuwa na ushawishi mkubwa wa kijeshi na kisiasa nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!