Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HABARI KUTOKA NIGERIA ZASEMA KUWA WALE WANAWAKE 60 WALIO SHIKILIWA NA KUNDI LA BOKO HARAMU HIVI MAJUZI,WAMETOROKA.

HABARI KUTOKA NIGERIA ZASEMA KUWA WALE WANAWAKE 60 WALIO SHIKILIWA NA KUNDI LA BOKO HARAMU HIVI MAJUZI,WAMETOROKA.

Written By Unknown on Monday, 7 July 2014 | Monday, July 07, 2014

Zaidi ya wanawake na wasichana sitini waliokuwa wakishikiliwa kwa zaidi ya wiki mbili na wanamgambo wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, wamefanikiwa kutoroka huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kiongozi mmoja wa kieneo katika mji wa Maiduguri makao makuu ya jimbo la Borno amesema kuwa, karibu wanawake na wasichana 63 siku ya Ijumaa walifanikiwa kutoroka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram na kurejea kwenye makazi yao. Kiongozi huyo amesema kuwa, wanawake hao walifanikiwa kutoroka mahala walipohifadhiwa wakati wanamgambo hao walipokuwa wakipambana na majeshi ya serikali.

Taarifa kutoka Maiduguri zinasema kuwa, wanamgambo 50 wa Boko Haram waliuawa siku ya Ijumaa baada ya kujiri mapigano kati yao na majeshi ya serikali ya Nigeria katika kitongoji cha Bambwa. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la Boko Haram bado lingali linawashirikilia wanafunzi wa kike wapatao 267 wa shule ya Chibok, waliotekwa nyara tokea mwezi Aprili uliopita.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi