Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SHAMBULIO JINGINE LATOKEA HUKO KENYAA,HII SASA WATU 29 WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA.

SHAMBULIO JINGINE LATOKEA HUKO KENYAA,HII SASA WATU 29 WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA.

Written By Unknown on Monday, 7 July 2014 | Monday, July 07, 2014

Kwa akali watu 29 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada ya watu wanaobeba silaha kufanya mashambulio katika maeneo mawili tofauti katika Kaunti za Lamu na Tana River, Pwani ya Kenya. Mwenda Njoka Msemaji wa Wizara ya Usalama wa Ndani wa Kenya amesema kuwa, wanamgambo wanaobeba silaha walilishambulia eneo la Hindi, lililoko umbali wa kilomita 15 kutoka Kaunti ya Lamu na kuuawa watu tisa. Njoka ameongeza kuwa, watu wengine 20 waliuawa kwenye shambulio lililofanywa katika eneo la Gamba lililoko karibu na Kaunti ya Tana River.

Wakati huohuo, Abdulaziz Abu Musab Msemaji wa al Shabab amesema kuwa, kundi hilo ndilo lililohusika na shambulio hilo. Kwa upande mwingine William Ruto Naibu wa Rais wa Kenya amevitaka vyombo vya usalama kuwasaka na kuwatia mbaroni watekelezaji wa shambulio hilo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, Grace Kaindi Naibu Inspekta wa Jeshi la Polisi la Kenya amelituhumu kundi la Mombasa Republican Council MRC kuwa ndilo lililohusika na shambulio hilo ambalo linatajwa kuwa linalotokana na msukumo wa kisiasa, kidini au mgogoro wa ardhi.


 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi