Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » BAADA YA WATU KUWA NA SHAKA NA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL HATIMAYE MKONGWE RONALDO (KISU) NA YEYE PIA AIKOSOA

BAADA YA WATU KUWA NA SHAKA NA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL HATIMAYE MKONGWE RONALDO (KISU) NA YEYE PIA AIKOSOA

Written By Unknown on Friday, 4 July 2014 | Friday, July 04, 2014

Aliyekuwa mchezaji bora duniani Ronaldo Luís Nazário de Lima, ameikosoa timu ya taifa ya Brazil kwa kusema bado kuna wachezaji wanacheza chini ya kiwango, hali ambayo inamuogopesha katika kipindi hiki cha michezo ya hatua ya mtoano inayoendelea kwenye michuano ya kombe la dunia.
Ronaldo, ambaye alikuwa mchezaji bora duniani kwa vipindi vitatatu tofauti na hiyo ilikuwa ni mwaka 1996, 1997 pamoja na 2002 amesema mpaka sasa anaona kuna mapungufu makubwa katika safu ya ushambuliaji ambayo haijatumikiwa ipasavyo.
Amesema mshambuliaji wa FC Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior ndiye mchezaji pekee anayempa matumaini kutokana na mchezo mzuri anaoendelea kuuonyesha, lakini kwa washambuliaji wengine kama Jo na Fred bado kuna mashaka kwake.
Katika hatua nyingine de Lima, amesema ana imani kubwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Luis Philipe Scolari atafanya mabadiliko kuelekea katika mchezo wa hii leo ambapo The Canarinho watakuwa wakicheza mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Colombia.

Mchezo mwingine wa hatua ya robo fainali ya kombe la dunia utakaochezwa hii leo ni kati ya timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya mabingwa wa soka wa dunia mwaka 1998 timu ya taifa ya Ufaransa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi