Home »
siasa afrika
» SOMA KILE ILICHO KISEMA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI LA (W.H.O) KUHUSIANA NA UGONJWA SUGU WA EBOLA UNAO ENDELEA KUMALIZA RAIA HUKO AFRICA YA MAGHARIBI.
SOMA KILE ILICHO KISEMA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI LA (W.H.O) KUHUSIANA NA UGONJWA SUGU WA EBOLA UNAO ENDELEA KUMALIZA RAIA HUKO AFRICA YA MAGHARIBI.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, homa ya ebola iliyozuka
katika eneo la magharibi mwa Afrika yataendelea kuua watu kwa miezi
kadhaa ijayo. Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa, watu wasiopungua 476
wameshafariki dunia magharibi mwa Afrika kutokana na kuambukizwa virusi
vya homa hiyo. Mamia ya raia wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa ebola
katika nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone huku juhudi za
kukabiliana na ugonjwa huo zikionekana kushindikana.

Wakati huo huo
mawaziri wa afya wan chi 11 za eneo la magharibi mwa Afrika
wamehitimisha kikao chao cha siku mbili katika mji mkuu wa Ghana Accra
na kupasisha mkakati wa pamoja wa kukabiliana mlipuko wa virusi vya
ebola. Ushirikiano wa pamoja mipakani, kuongeza usimamizi zaidi wa
kugundua maradhi ya ebola na kuimarisha ushirikiano na Shirika la Afya
Duniani WHO ni sehemu tu ya mikakati iliyokubaliwa na mawaziri wan chi
11 za magharibi mwa Afrika kama moja ya njia za kupambana na homa ya
ebola. Hakuna tiba ya homa ya Ebola ambayo dalili zake ni kuharisha,
kutapika na kutokwa damu katika sehemu mbalimbali mwilini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!