Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WAISLAM KADHAA WAMEUWAWA HUKO MYANMAR BAADA YA KUNDI LA WABUDHAA KUWASHAMBULIA.

WAISLAM KADHAA WAMEUWAWA HUKO MYANMAR BAADA YA KUNDI LA WABUDHAA KUWASHAMBULIA.

Written By Unknown on Friday, 4 July 2014 | Friday, July 04, 2014

Polisi ya Myanmar ametangaza kuwa, kwa akali watu wawili wameuawa kwenye mapigano mapya kati ya Mabudha na Waislamu katika mji wa Mandalay, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo. Polisi ya Myanmar imeeleza kuwa, mapigano hayo yalitokea baada ya Mabudha kushambulia duka linalomilikiwa na Muislamu katika mji huo.
Polisi ilitumia risasi za plastiki kuwatawanya Mabudha waliokuwa wamejizatiti na visu, marungu na mawe.
Mkuu wa Polisi katika mji wa Mandalay amesema kuwa, uchunguzi umeshaanza ili kubaini watu waliohusika na shambulio hilo dhidi ya Waislamu. Wimbi la mashambulio ya Mabudha dhidi ya Waislamu lilianza mwaka 2012, yaliyopelekea zaidi ya watu 250 kuuawa na zaidi ya laki moja na elfu arobaini wengi wao wakiwa Waislamu kuwa wakimbizi. Waislamu nchini Myanmar wanaunda asilimia nne ya wakazi wote nchini humo.
Mashambulio na mauaji dhidi ya Waislamu yanatokea katika hali ambayo, Watawa wa Kibudha wenye misimamo ya kufurutu ada wamekuwa wakiwashawishi wananchi wa nchi hiyo kususia bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Waislamu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi